Almasi

Almasi katika hali asilia kabla ya kukatwa na kusuguliwa
Almasi dukani zilizosuguliwa na kung'arishwa tayari

Almasi ni vito adimu vyenye thamani kubwa.

Mara nyingi hazionyeshi rangi lakini kuna pia almasi za njano, buluu au nyekundu. Zinatumiwa kama mapambo na kutokana ugumu wao pia katika teknolojia ya kukata.

Kaboni iliyobadilika

[hariri | hariri chanzo]

Kikemia almasi ni umbo moja la kaboni (C) tupu katika hali ya fuwele ni dutu ileile kama makaa. Ila tu kaboni huwa almasi katika mazingira ya joto kali na shindikizo kubwa. Badiliko hili latokea kwa kawaida katika ganda la dunia kwenye kina cha kilomita 150 karibu na volkeno.

Almasi sintetiki

[hariri | hariri chanzo]

Kwa matumizi ya kiteknolojia almasi ndogo hutengenezwa kwa kutumia mashine zinazosukuma kaboni kwa shindikizo kubwa na halijoto ya 1,500 °C hadi kuwa almasi sintetiki yenye tabia zote za almasi asilia. Maendeleo ya teknolojia yamewezesha pia kupatikana kwa almasi sintetiki zinazofaa pia kama mapambo.

Madini ngumu duniani

[hariri | hariri chanzo]

Almasi ni dutu ngumu kabisa inayopatikana duniani kushinda metali au madini yote. Hii ni sababu ya kwamba almasi zinatumiwa katika teknolojia mbalimbali. Vyombo vya kukata aloi ngumu sana za feleji au keekee za kutoboa mwamba wakati wa kutafuta mafuta ya petroli vyote vyatumia vipande vya almasi.

Almasi yenyewe hukatwa kwa unga wa almasi tu.

Kampuni kubwa duniani ya kuchimba almasi na kufanya biashara nazo ni De Beers wa Afrika Kusini.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Almasi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.