Blaise Pascal

Blaise Pascal
Taswira ya Blaise Pascal
Taswira ya Blaise Pascal
Alizaliwa 19 Juni 1623
Alikufa 19 Agosti 1662
Nchi Ufaransa
Kazi yake mtaalamu wa falsafa,
hisabati, na teolojia

Blaise Pascal alikuwa mtaalamu mashuhuri wa hisabati, falsafa na teolojia kutoka nchi ya Ufaransa.

Alizaliwa huko Clermont-Ferrand, mkoa wa Auvergne.

Alipokuwa na umri wa miaka 3 alifiwa na mama, Antoinette Begon. Hapo baba yake, Étienne Pascal (1588 - 1651), wakili na mwanahisabati, alishughulikia mwenyewe malezi yake.

Mtoto Blaise alionyesha mapema uwezo wake mkubwa katika masomo, hasa ya hisabati na fizikia, hata akakaribishwa katika mikutano ya kisayansi iliyoongozwa na Marin Mersenne, aliyekuwa na mawasiliano na wansayansi bora wa wakati huo, kama vile Girard Desargues, Galileo Galilei, Pierre de Fermat, René Descartes na Evangelista Torricelli.

Tangu 1639 hadi 1647 aliishi Rouen, ambapo baba yake alipewa kazi fulani na kardinali Armand-Jean du Plessis de Richelieu. Huko, mwaka 1640, Blaise Pascal alitunga kitabu chake cha kwanza (Essai pour les coniques), na mwaka 1644 alitengenwa mashine yake ya kwanza kalkuleta. Tena mwaka 1646, pamoja na baba yake na ndugu zake alikumbatia itikadi kali ya dini ya Kikristo ya Wajanseni.

Kutokana na afya mbaya, mwaka 1650, Pascal aliacha masomo ya hisabati mpaka mwaka 1653, alipoandika Traité du triangle arithmétique, alipofafanua pembetatu inayobeba jina lake.

Kisha kunusurika kiajabu katika ajali ya mwaka 1654, Pascal aliacha moja kwa moja masomo ya hisabati na fizikia ili kukazania falsafa na teolojia. Tangu hapo alijiunga na marafiki wa abasia ya Port-Royal, iliyoanzishwa na askofu Janseni, akashiriki katika mabishano kati ya wafuasi wa askofu huyo mwenye itikadi kali na wanateolojia wa chuo kikuu cha Sorbone huko Paris.

Miaka 1656 na 1657, akitumia jina la bandia Louis de Montalte, alitolea barua zake za kwanza kwa rafiki yake mmojawapo kuhusu mabishano hayo. scritte da un provinciale ad uno dei suoi amici, sulle dispute della Sorbona. Lakini mwaka 1660, mfalme Alois XIV aliagiza ziteketezwe zote.

Lakini, wakati wa kuandika hizo "Barua toka mkoani", Pascal aliwaza kuandika kitabu kirefu zaidi cha kutetea Ukristo, mbali ya Ujanseni. Lakini afya yake mbovu ilikuwa imeharibika zaidi, hata akafa tarehe 19 Agosti 1662, akiwa na miaka 39 tu.

Miniti ya barua zake ilikusanywa na ndugu na marafiki katika kitabu maarufu kwa jina la Mawazo, mchanganyiko wa falsafa, maadili na teolojia unaotetea Ukristo.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]