Historia ya Slovenia
Historia ya Slovenia inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Slovenia.
Waslavi walihamia Slovenia ya leo katika karne ya 6 BK na kuipatia jina hilo.
Tangu zamani wakazi waliishi chini ya utawala wa madola mbalimbali kama vile Dola la Roma, Austria na Yugoslavia hadi kupata uhuru wa kisiasa mara ya kwanza kabisa mwaka 1991 baada ya mwisho wa Shirikisho la Yugoslavia.
Kati ya nchi zote zilizotokana na Yugoslavia ya zamani Slovenia ni nchi yenye uchumi imara zaidi, tena haikuathiriwa na vita vya kikabila vilivyoharibu majimbo mengine, hivyo ikawahi kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Slovenia kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |