Karolo Lwanga
Karoli Lwanga (Bulimu, 1865 - Namugongo, 3 Juni 1886) ndiye maarufu zaidi kati ya wafiadini wa Uganda waliouawa kwa amri ya kabaka Mwanga II (dhuluma za miaka 1885 - 1887).
Pamoja na wenzake anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Wote pamoja walitangazwa na Papa Benedikto XV kuwa wenye heri tarehe 6 Juni 1920, halafu na Papa Paulo VI kuwa watakatifu tarehe 8 Oktoba 1964.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Juni[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Alikuwa mkuu wa wahudumu katika ikulu ya mfalme wa Buganda: kisha kumuamini Yesu Kristo na kubatizwa na Wamisionari wa Afrika wa kardinali Charles Lavigerie, alitetea kwa ushujaa imani hiyo na maadili yanayotokana nayo akiwahimiza mpaka mwisho wenzake kudumu waaminifu hadi kifodini kilichowapata baadhi kwa upanga na baadhi kwa kuchomwa moto.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Wafiadini wa Uganda
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- J. FRANSE, W.F., Mashahidi 22 wa Uganda – tafsiri ya C. Kuhenga n.k. – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1981
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Charles Lwanga and Companions Archived 7 Juni 2008 at the Wayback Machine.
- Charles Lwanga and Companions Archived 29 Machi 2009 at the Wayback Machine.
- The Uganda Martyrs from the August 2008 issue of The Word Among Us magazine
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |