Kilomita ya mraba
Kilomita ya mraba (km²) ni kipimo cha eneo; eneo lenye upana na urefu wa kilomita moja
Msingi wake ni mita ya mraba (m²). Kilomita ya mraba hutumika kwa upimaji wa maeneo makubwa duniani kama mji, mkoa, nchi au dunia yote.
Kilometa 1 ya mraba (km²) ni sawa na:
- eneo la mraba yenye urefu wa kilomita moja kila upande
- Mita ya mraba 1,000,000
- Hektari 100
- Ekari 247.105 381
- Maili ya mraba 0.386 102
Au:
- Mita ya mraba 1 = kilometa ya mraba (km²) 0.000 001
- Hektari 1= kilometa ya mraba (km²) 0.01
- Maili ya mraba 1 = kilometa ya mraba 2.589 988
- Ekari 1 = kilometa ya mraba 0.004 047