Kilwa
Kilwa ni jina la wilaya na mahali patatu katika mkoa wa Lindi, Tanzania.
- Wilaya ya Kilwa iko kati ya Dar-es-salaam na Lindi ufukoni wa Bahari Hindi.
- Kilwa Masoko ni makao makuu ya wilaya.
- Kilwa Kivinje ni mji wa kihistoria tangu karne ya 18.
- Kilwa Kisiwani ni kisiwa karibu na mwambao kinachotazama Kilwa Masoko. Hapo ndipo Kilwa ya kihistoria iliyojulikana kama mji mkubwa wa pwani ya Afrika ya Mashariki tangu nusu ya kwanza ya karne ya 14 BK kutokana na taarifa ya msafiri Ibn Battuta. Pamoja na mabaki ya mji wa Songo Mnara, magofu ya Kilwa Kisiwani yameandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).
Kuna pia kata inayoitwa Kilwa katika Wilaya ya Kilindi, Mkoa wa Tanga, Tanzania.