Mkia
Mkia ni sehemu ya mwisho ya uti wa mgongo kwenye mwili wa wanyama wengi wa vertebrata. Jina hilo latumiwa pia kwa wanyama wengine wenye upanuzi mwembamba wa mwili upande wa nyuma na pia kutaja sehemu nyembamba ya nyuma kwa vitu mbalimbali.
Vertebrata
[hariri | hariri chanzo]Kwa vertebrata mkia ni sehemu ya uti wa mgongo inayoelekea nje ya pingiti inayokwisha kwenye mkundu. Mifupa ya mkia hufunikwa na musuli na ngozi, mara nyingi pia na nywele, manyoya au magamba.
Vertebrata wengine wana musuli nyingi na hivyo nguvu kubwa kwenye mkia, kwa mfano nyani wanaotumia mkia kama mkono wakiweza kushika tawi la mti na kutundika hapo kwa nguvu ya mkia pekee. Wanyama wengine wana mkia mdogo tu. Binadamu na chura wana mkia wakiwa katika hali ya kiinitete lakini unapotea baadaye. Watu wachache huzaliwa wakiwa bado na mkia mdogo.
Wanyama kama paka na mbwa hutumia mkia kwa ajili ya mawasiliano, kuna "lugha" ya mkia.
Kuna aina za mjusi zinazoweza kuachana na mkia wao zikishambuliwa na kushikwa na adui mkubwa.
Wanyama wengine
[hariri | hariri chanzo]Wanyama wasio na uti wa mgongo wanaweza kuwa na sehemu ya nyuma inayoonekana kuwa nyuma ya pingiti. Mfano ni nge anayebeba mwiba wa sumu hapo.
"Mkia" wa mitambo na mengine
[hariri | hariri chanzo]Kama mashine au mtambo mwingine ina upanuzi mwembamba wa nyuma, sehemu hizi mara nyingi zinaitwa "mkia" pia. Mfano ni sehemu ya nyuma ya eropleni.
Nyotamkia zinaonekana kama nukta ya nuru, yaani nyota yenye upanuzi nyuma na hapo ni asili ya jina "nyota yenye mkia".
Picha za mkia
[hariri | hariri chanzo]- Nguruwe (Sus domestica)
- Glyptodon (Glyptodon asper)
- Samaki (Lactoria cornuta)
- Pundamilia (Equus grevyi)
- Mamba (Alligator mississipiensis)
- Kiboko (Hippopotamus amphibius)
- Picha ya mtoto mwenye mkia (mnamo 1925)
- Nyotamkia C1911 01
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkia kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |