Msimamizi

"Dirisha la Ubatizo" katika St. Mary's Episcopal Cathedral in Memphis, Tennessee, likionyesha wasimamizi katika ubatizo.

Msimamizi (kutoka kitenzi: kusimama) ni mtu ambaye anasimama imara kuhakikisha mwingine anakua vizuri au jambo linafanyika kwa ufanisi, kwa mfano mirathi.

Katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo ni maarufu wasimamizi wa ubatizo na wa kipaimara wanaowajibika rasmi, wakati wa kuadhimisha sakramenti hizo, kwamba atamsaidia aliyezipata kuziishi vema maisha yake yote.

Katika baadhi ya madhehebu hayo, wanaoheshimiwa kama watakatifu wanatazamwa pia kama wasimamizi wa aina fulani ya watu, k.mf. vijana, wajane, wakoma n.k.

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msimamizi kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.