Baharia
Baharia (pia mwanamaji. hasa kwa kutaja mabaharia wa kijeshi) ni mtu anayefanya kazi kwenye chombo cha usafiri majini, hasa baharini kama vile boti, mashua, jahazi au meli. Mkuu wao ni nahodha au kapteni wa chombo.
Kuna kazi nyingi tofauti zinazotekelezwa na mabaharia. Katika mashua au jahazi ndogo mabaharia wote wanafanya kazi pamoja ilhali kazi sahili na ngumu zaidi hupewa kwa wale walio vijana. Kadri jinsi meli ni kubwa zaidi shughuli zinagawiwa baina ya mabaharia wenye ufundi fulani.
Meli kubwa unaweza kuwa na idara tofauti kama vile
Hapo kapteni atakuwa na kundi la maafisa wake wanaosimamia idara mbalimbali baada ya kupitia mafunzo na mitihani maalumu kwa ajili ya shughuli zao.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Survey of Water Transport Occupations Archived 29 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- Seafarer Fatigue: The Cardiff Research Programme Archived 31 Machi 2007 at the Wayback Machine.
- Sailor at Etymology Online
- The Telegraph, Sea no evil: the life of a modern sailor