Nitrojeni
Nitrojeni (Nitrogenium) | |
---|---|
Nitrojeni ndani ya chombo katika hali ya kiowevu ikiwa na halijoto chini ya -182.95 °C | |
Jina la Elementi | Nitrojeni (Nitrogenium) |
Alama | N |
Namba atomia | 7 |
Mfululizo safu | Simetali |
Uzani atomia | 14.0067 |
Valensi | 2, 5 |
Densiti | 1.251 g/L |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 63.15 K (−210.00 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 77.36 K (−195.79 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 0,03 % |
Hali maada | gesi |
Nitrojeni ni elementi yenye namba atomia 7 katika mfumo radidia na uzani atomia 14.0067. Alama yake ni N. Ina elektroni 5 katika ganda la nje.
Duniani haipatikani kama atomi za pekee lakini kama molekuli ya N2 inayounganisha atomi mbili za N. Katika hali hii ni gesi isiyo na ladha au harufu. Gesi hii ni sehemu kubwa ya hewa tunayopumua ambamo kuna asilimia 78 za nitrojeni na 21 % za oksijeni.
Nitrojeni imo ndani ya kila kiumbehai hakuna uhai duniani bila N. Shambani huongezwa kama mbolea kwa kukuza mimea.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Mfumo radidia
- Orodha ya elementi
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nitrojeni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |