Pasaka

Meza ya Seder yaani Chakula cha Pasaka ya Kiyahudi ikionyesha vitabu vya Haggada.
Yesu mfufuka.
Mayai ya Pasaka.

Pasaka ni sikukuu muhimu katika dini za Uyahudi na Ukristo. Jina la Pasaka limetokana na neno la Kiebrania "פסח" (tamka: pasakh).

Taarifa za Agano Jipya zinatoa habari ya kuwa kufa na kufufuka kwa Yesu yametokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi. Kwa hiyo jina la sikukuu hiyo limeendelea kutumika kwa ajili ya sherehe ya Kikristo.

Tarehe ya Pasaka

Pasaka ni sikukuu inayobadilika tarehe yake katika kalenda ya kawaida kila mwaka.

Pasaka ya Kiyahudi inafuata kalenda ya Kiyahudi: ni tarehe 15 Nisan ambayo ni siku baada ya mwezi mpevu wa kwanza baada ya sikusare ya machipuko (mnamo 21 Machi).

Kwa kawaida Pasaka ya Kikristo, tangu karne ya 1 au karne ya 2 inaunganisha siku ya Jumapili (ni Jumapili kila mwaka kwa sababu ndiyo siku ya ufufuko katika mapokeo ya Kikristo) pamoja na kumbukumbu ya pasaka ya Kiyahudi.

Tangu mtaguso wa kwanza wa Nikea Wakristo walipatana kusheherekea Pasaka kwenye Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu unaotokea baada ya sikusare ya tarehe 21 Machi. Kwa hiyo Pasaka inaweza kutokea kati ya 22 Machi hadi 25 Aprili.

Tangu masahihisho ya kalenda ya Juliasi na kuanzishwa kwa kalenda ya Gregori mara nyingi kuna tofauti kati ya Pasaka ya Ukristo wa magharibi (sehemu kubwa ya Kanisa Katoliki na makanisa ya Uprotestanti) na Pasaka ya Ukristo wa mashariki kwa sababu Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda ya Juliasi kwa ajili ya kukadiria sikukuu zao.

Majina ya Pasaka ya Kiyahudi na Pasaka ya Kikristo katika lugha mbalimbali

Katika lugha nyingi, asili hii bado inaonekana, ingawa mara nyingi umbo la neno ni tofauti kidogo. Jina la sikukuu ya Kiyahudi linapatikana kwa maumbo mbalimbali. Siku hizi mara nyingi umbo la neno la Kiebrania limetumika lakini desturi katika lugha hizo inaonyesha pia umbo linalofanana zaidi na neno kwa ajili ya sherehe ya Kikristo.

Lugha Jina la Pasaka ya Kiyahudi Jina la Pasaka ya Kikristo
Kifaransa Pessah Paque; Les Paques
Kihispania pascua pascua
Kiitalia Pasqua ebraica; Pesach; Pesah Pasqua
Kipoland Pesach Wielkanoc; Pascha
Kirusi Пасха; Песах (pas-kha; pesakh) Пасха (pas-kha)
Kigiriki Πάσχα (pas-kha) Πάσχα (pas-kha)
Kidenmark Pesach Påske
Kinorwei Pesah Påske
Kiswidi Pesach;Påsk Påsk
Kiholanzi Pesach Pasen
Kijerumani Passah Ostern
Kiingereza Passover Easter
Kiajemi پسح

پاک

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Liturujia

Desturi

Hesabu

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.