Tumati

Tumati ni kata ya Wilaya ya Mbulu Vijijini katika Mkoa wa Manyara, Tanzania.

Kata hii ipo katika uwanda wa juu na inapakana na msitu mnene wa Nowu kwa upande wa mashariki, kaskazini kata ya Yaeda Ampa, magharibi kata ya Dongobesh na kusini wilaya ya Babati. Eneo kubwa la kata hii lina baridi kali mwaka mzima, hasa vijiji vya Tumati, Mongahay na Endesh.

Kata ya Tumati inajumuisha vijiji vya Tumati, Mongahay, Endoji, Endesh na Getesh.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 14,745 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,798 waishio humo.[2]

Wenyeji wa kata hii ni wa kabila la Wairaqw kwa zaidi ya asilimia 98.

Kilimo ndiyo shughuli kubwa katika kata hii; mazao yalimwayo ni mahindi, maharage, viazi mviringo na vitunguu saumu ambapo wenyeji wanayaita mashamba ya zao hili kuwa ni "migodi" au "nyumba za kupanga" kutokana na fedha nyingi zinazotokana na zao hilo. Mbali na kilimo wenyeji pia wanajishughulisha na ufugaji.

Kata hii ni miongoni mwa kata zilizoongoza Tanzania kuwa na shule nyingi za wananchi za kata. Kabla ya kata kugawanywa mwaka 2009 ilkuwa na shule 3 za sekondari za wananchi shule hizo ni Tumati, Yaeda Ampa na Endoji. Kwa sasa zipo shule 2 za Tumati na Endoji baada ya shule ya Yaeda Ampa kuwa katika kata mpya ya Yaeda Ampa. Zipo shule 7 za msingi ambazo ni Tumati, Mongahay, Yerotamburda, Endesh, Endoji, Erboshan na Getesh.

Kata za Wilaya ya Mbulu Vijijini - Mkoa wa Manyara - Tanzania

Bashay | Dinamu | Dongobesh | Endahagichan | Endamilay | Eshkesh | Geterer | Gidhim | Haydarer | Haydom | Labay | Maghang | Maretadu | Masieda | Masqaroda | Tumati | Yaeda Ampa | Yaeda Chini


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tumati kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.