Kura ya turufu
Kura ya turufu (kimataifa mara nyingi Veto (kwa Kilatini "ninakataza") ni haki ya kukataza azimio lisipite wala kutekelezwa hata kama limekubaliwa na wengi.
Veto ya rais dhidi ya bunge
[hariri | hariri chanzo]Katika nchi nyingi rais au kiongozi wa taifa kwa manufaa ya taifa ana haki ya kukataza maazimio au sheria zilizokubaliwa na bunge akiona kasoro au hasara ndani yake.
Kwa mfano nchini Marekani rais ana haki ya kukataza kila sheria iliyokubaliwa na bunge katika kipindi cha siku 10 baada ya azimio la bunge. Akipiga veto sheria inarudi bungeni. Hapo bunge linaweza kufuta veto kwa theluthi mbili za kura zake au bunge linaweza kubadilisha sheria hadi kupatana na mapenzi ya rais.
Kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa
[hariri | hariri chanzo]Mataifa matano yanaweza kutumia kura ya turufu (veto) katika Baraza la Usalama la UM: ni China, Marekani, Ufaransa, Uingereza na Urusi. Kila moja kati ya hayo linaweza kuzuia maazimio yoyote ya baraza la usalama.
Asili katika historia
[hariri | hariri chanzo]Asili ya neno "veto" iko katika lugha ya Kilatini. Katika Roma ya Kale kulikuwa na afisa mmoja mwenye kuwakilisha wananchi wa kawaida mbele ya senati ya Roma. Kama maseneta ambao wote walitoka katika familia za makabaila walitoa maamuzi ya kuathiri vibaya hali ya raia huyu mwakilishi alikuwa na haki ya kupiga veto, na hivyo kuzuia azimio.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Regular Vetoes and Pocket Vetoes: An Overview (report) by Kevin R. Kosar
- Senate Reference Webpage on Vetoes, which includes lists of vetoes from 1789 to the current day.