Uhusika milikishi
Uhusika milikishi (en:Genitive case) ni istilahi ya sarufi za lugha za Kihindi-Kiulaya na nyinginezo inayotaja hali ya neno, hasa nomino, kuwa na nomino nyingine.
Katika Kiswahili hali kama hii inatajwa kwa kutumia -a kama kiunganishi, kwa mfano "nyumba ya baba"; kwa Kilatini "domus patri" ambako "patri" ni uhusika milikishi wa "pater" (baba). Kiingereza imeshapotewa na uhusika huu, hivyo kinatumia "father's house". Kumbe lugha za Kijerumani, Kigiriki na lugha za Kibaltiki zinaendelea kutumia uhusika milikishi.
Matumizi yake yanaeleza badiliko la umbo la neno katika majina ya kisayansi pale ambapo majina yametoka katika lugha ya Kilatini au Kigiriki. Mfano ni majina ya nyota. Nyota angavu zaidi katika kundinyota la "Centaurus" huitwa "Alfa Centauri" ilhali "Centauri" ni uhusika milikishi wa "centaurus". Vile vile "Alfa Leonis" kwa nyota angavu katika kundinyota la "Leo" ("Simba", taz. Asadi).
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uhusika milikishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |