Urano
Urano | |
---|---|
Mungu wa mbingu | |
Makao | Mbinguni |
Mwenzi | Gaya |
Wazazi | Gaya |
Ndugu | Ponto |
Watoto | Titani Kumi na Wawili, Siklopsi, Nimfa-miti, Furia Watatu, Giganti na Afrodita |
Ulinganifu wa Kirumi | Caelus |
Urano au Uranos (kwa Kigiriki Οὐρανός, ouranos) alikuwa mungu wa mbingu katika dini ya Ugiriki ya Kale. Mama yake alikuwa mungu wa kwanza Gaya ambaye ni ardhi yenyewe.
Baadaye alianza kuzaliana na mamake kizazi cha pili cha miungu katika Mitholojia ya Kigiriki: kati hao kundi walioitwa Watitani.
Kutoka wale Titani ni mdogo wao Kronos aliyempindua baba na kuwa mkuu wa miungu hadi mwenyewe alipopinduliwa na Zeu.
Analingana na Caelus katika dini ya Roma ya Kale.
Jina la mungu huyu lilichaguliwa katika karne ya 19 kuitaja sayari ya saba Uranus baada ya sayari hii kugunduliwa na mwanafalaki Herschel kwa kutumia mitambo ya kisasa ya wakati wake.