Kwale (ndege)
Kwa maana nyingine ya jina hili angalia hapa
Kwale | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kwale miguu-njano (Peliperdix coqui) | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 6 za kwale:
|
Kwale (pia kware) ni ndege wa jenasi mbalimbali katika nusufamilia Perdicinae wa familia ya Phasianidae. Spishi za jenasi Pternistis zinatambuliwa kuwa na nasaba mbali kidogo na jenasi nyingine. Ingawa watu wengi huwaita kwale, sasa jina kereng'ende linapendelewa. Rangi ya kwale ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Mara nyingi miguu yao ni myekundu au rangi ya manjano na koo lao ni jekundu, jeupe, jeusi au rangi ya manjano. Hujificha kwa kawaida lakini sauti yao husikika mara kwa mara. Chakula chao ni mbegu, wadudu na nyungunyungu. Hutaga mayai matatu hadi kumi ardhini pengine juu ya manyasi makavu.
Karibu spishi zote zinatokea Afrika lakini spishi tano zinatokea Asia.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Campocolinus dewittei, Kwale Kidari-kahawianyekundu (Chestnut-breasted Francolin)
- Campocolinus spinetorum, Kwale Tumbo-njano (Pale-bellied Francolin)
- Campocolinus maharao, Kwale Tumbo-mabaka (Bar-bellied Francolin)
- Campocolinus hubbardi, Kwale Tumbo-jeupe (Plain-bellied Francolin)
- Campocolinus thikae, Kwale wa Thika (Thika Francolin)
- Campocolinus stuhlmanni, Kwale wa Stuhlmann (Stuhlmann’s Francolin)
- Dendroperdix grantii, Kwale wa Grant (Grant's Francolin)
- Dendroperdix rovuma, Kwale wa Kirk (Kirk's Francolin)
- Dendroperdix sephaena, Kwale Kishungi (Crested Francolin)
- Francolinus pondicerianus, Kwale wa Uhindi (Grey Francolin) imewasilishwa katika Shelisheli na Saint Helena
- Peliperdix albogularis, Kwale Koo-jeupe (White-throated Francolin)
- Peliperdix coqui, Kwale Miguu-njano (Coqui Francolin)
- Peliperdix lathami, Kwale-misitu (Latham's Francolin)
- Peliperdix schlegelii, Kwale wa Schlegel (Schlegel's Francolin)
- Pternistis adspersus, Kereng'ende Domo-jekundu (Red-billed Spurfowl)
- Pternistis afer, Kereng'ende Koo-jekundu (Red-necked Spurfowl)
- Pternistis ahantensis, Kereng'ende wa Ahanta (Ahanta Spurfowl)
- Pternistis atrifrons, Kereng'ende Paji-jeusi (Black-fronted Spurfowl)
- Pternistis bicalcaratus, Kereng'ende Vikwaru-viwili (Double-spurred Spurfowl)
- Pternistis camerunensis, Kereng'ende wa Kameruni (Mount Cameroon Spurfowl)
- Pternistis capensis, Kereng'ende Kusi (Cape Spurfowl)
- Pternistis castaneicollis, Kereng'ende Kisogo-chekundu (Chestnut-naped Spurfowl)
- Pternistis clappertoni, Kereng'ende wa Clapperton (Clapperton's Spurfowl)
- Pternistis cranchii, Kereng'ende wa Cranch (Cranch’s Spurfowl)
- Pternistis erckelii, Kereng'ende wa Erckel (Erckel's Spurfowl)
- Pternistis griseostriatus, Kereng'ende Michirizi-kijivu (Grey-striped Spurfowl)
- Pternistis hartlaubi, Kereng'ende wa Hartlaub (Hartlaub's Spurfowl)
- Pternistis harwoodi, Kereng'ende wa Harwood (Harwood's Spurfowl)
- Pternistis hildebrandti, Kereng'ende wa Hildebrandt (Hildebrandt's Spurfowl)
- Pternistis icterorhynchus, Kereng'ende wa Heuglin (Heuglin's Spurfowl)
- Pternistis jacksoni, Kereng'ende-milima (Jackson's Spurfowl)
- Pternistis leucoscepus, Kereng'ende Koo-njano (Yellow-necked Spurfowl)
- Pternistis natalensis, Kereng'ende wa Natal (Natal Spurfowl)
- Pternistis nobilis, Kereng'ende Mrembo (Handsome Spurfowl)
- Pternistis ochropectus, Kereng'ende wa Jibuti (Djibouti Spurfowl)
- Pternistis rufopictus, Kereng'ende Kidari-kijivu (Grey-breasted Spurfowl)
- Pternistis schuetti, Kereng'ende wa Schütt (Schuett’s Spurfowl)
- Pternistis squamatus, Kereng'ende Mabaka (Scaly Spurfowl)
- Pternistis swainsonii, Kereng'ende wa Swainson (Swainson's Spurfowl)
- Pternistis swierstrai, Kereng'ende wa Swierstra (Swierstra's Spurfowl)
- Scleroptila afra, Kwale Mabawa-kijivu (Grey-winged Francolin)
- Scleroptila crawshayi, Kwale wa Crawshay (Crawshay’s Francolin)
- Scleroptila elgonensis, Kwale wa Elgon (Elgon Francolin)
- Scleroptila finschi, Kwale wa Finsch (Finsch's Francolin)
- Scleroptila gutturalis, Kwale wa Kulal (Archer's Francolin)
- Scleroptila jugularis, Kwale wa Kunene (Kunene Francolin)
- Scleroptila levaillantii, Kwale Mabawa-mekundu (Red-winged Francolin)
- Scleroptila psilolaema, Kwale-mabwawa (Moorland Francolin)
- Scleroptila shelleyi, Kwale wa Shelley (Shelley's Francolin)
- Scleroptila streptophora, Kwale Shingo-nyeusi (Ring-necked Francolin)
- Scleroptila uluensis, Kwale wa Ulu (Ulu Francolin)
- Scleroptila whytei, Kwale koo-jekundu (Rufous-throated Francolin)
Spishi za Asia
[hariri | hariri chanzo]- Francolinus francolinus (Black Francolin)
- Francolinus gularis (Swamp Francolin)
- Francolinus pictus (Painted Francolin)
- Francolinus pintadeanus (Chinese Francolin)
- Francolinus pondicerianus (Grey Francolin)
Picha
[hariri | hariri chanzo]- Kwale kishungi
- Kwale wa Uhindi
- Kwale koo-jeupe
- Kereng'ende domo-jekundu
- Kereng'ende shingo-nyekundu
- Kereng'ende vikwaru-viwili
- Kereng'ende kusi
- Kereng'ende kisogo-chekundu
- Kereng'ende wa Erckel
- Kereng'ende wa Hartlaub
- Kereng'ende wa Heuglin
- Kereng'ende-milima
- Kereng'ende shingo-njano
- Kereng'ende wa Natal
- Kereng'ende mrembo
- Kereng'ende kidari-kijivu
- Kereng'ende mabaka
- Kereng'ende wa Swainson
- Kwale mabawa-kijivu
- Kwale wa Kulal
- Kwale mabawa-mekundu
- Kwale wa Shelley
- Black francolin
- Swamp francolin
- Painted francolin
- Grey francolin